Kuhusu Shule ya Sekondari Kajunguti
Shule ya Sekondari Kajunguti ni shule binafsi inayotoa elimu ya sekondari kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne (I–IV), kwa wanafunzi wa kike na wa kiume wanaosoma kwa mfumo wa bweni.
Shule ya Sekondari Kajunguti ilianzishwa rasmi mwezi Januari mwaka 2002 na Jumuiya ya Maendeleo Kajunguti (Kajunguti Development Association – KADA). Tangu kuanzishwa kwake, shule imeendelea kutoa mazingira bora na thabiti ya kitaaluma, yakilenga kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora na kufikia malengo yao.
Shule ya Sekondari Kajunguti ipo katika Kata ya Ihembe, Tarafa ya Nyaishozi, takribani kilomita 20 kutoka mji mdogo wa Omurushaka na kilomita 8 kutoka Nyaishozi Stesheni.
Shule ina mazingira mazuri na salama ya kujifunzia, ikiwemo umeme wa gridi ya taifa, upatikanaji wa maji ya uhakika pamoja na walimu wenye weledi na uzoefu katika kufundisha masomo mbalimbali.
Shule ya Sekondari Kajunguti ipo katika Kata ya Ihembe, Tarafa ya Nyaishozi, takribani kilomita 20 kutoka mji mdogo wa Omurushaka na kilomita 8 kutoka Nyaishozi Stesheni.
Dira ya shule
Kuhakikisha tunatoa jamii yenye elimu, uwezo na moyo wa maendeleo.
Mwelekeo wa Shule
Kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata maarifa, utaalamu na mwelekeo wa kimaendeleo na kupambana na changamoto
Malengo ya shule
Shule ya sekondari Kajunguti ina malengo, na haya ni baadhi ya malengo makuu ya shule.
Kutoa Elimu yote kwa ujumla ili kumpa mwanafunzi utaalamu wa kimaisha, taaluma, ufundi na nidhamu kwa vijana
Kuinua viwango vya taaluma kwa wanafunzi kwa kuboresha ufundishaji na usomaji darasani
Kutoa nafasi bora za masomo kwa gharama nafuu kwa watu wa rika zote mfano mpango wa Elimu ya watu wazima.
Maadili ya Shule
Katika Shule ya Sekondari Kajunguti, kila mwanajamii, wakiwemo wanafunzi na wafanyakazi, anatarajiwa kuzingatia na kuishi kwa kuzingatia maadili yafuatayo:
Ubora na Mafanikio
Tunawahimiza wanafunzi wetu kujifunza kwa bidii na kujitahidi kufikia viwango vya juu zaidi vya kibinafsi na kitaaluma.
Uadilifu na Uaminifu
Kujenga uaminifu, ukweli na tabia njema katika kila jambo tunalofanya, huku kila mwanajumuiya akizingatia maadili, uwajibikaji na heshima kwa wengine.
Heshima
Kuheshimu nafsi, wengine, mali na mazingira kwa ujumla. Kila mwanajumuiya anapaswa kutumia kwa uangalifu rasilimali na huduma za shule, ikiwemo maji, umeme na vifaa vya shule, kwa manufaa ya wote.
Uwajibikaji
Kuwajibika kwa matendo, maamuzi na majukumu yetu, na kuwa tayari kutambua wajibu wetu, kujifunza kutokana na makosa na kuchukua hatua sahihi kwa maendeleo binafsi na ya shule.
Ustahimilivu na Uvumilivu
Kujenga moyo wa kuvumilia na kutokata tamaa unapokutana na changamoto. Tunawahimiza wanafunzi kujifunza kutokana na makosa, kukubali changamoto kama sehemu ya kujifunza na kuendelea kujitahidi kwa mtazamo chanya hadi kufikia malengo yao.
Fadhili na Huruma
Kukuza upendo, huruma, kujali na kuheshimiana, kwa kujenga mahusiano mazuri na kusaidiana miongoni mwa wanafunzi, walimu na wanajumuiya wote wa shule.
Ushirikiano na Kazi ya Pamoja
Kufanya kazi pamoja kwa umoja, ushirikiano na kuheshimiana, tukitambua na kuthamini uwezo wa kila mmoja. Tunashirikiana kwa kutumia nguvu zetu pamoja na kusaidiana pale tunapokutana na changamoto ili kufikia mafanikio ya pamoja.
Udadisi na Kujifunza
Kukuza shauku ya kujifunza, udadisi na upatikanaji wa maarifa mapya, huku tukiwahimiza wanafunzi kuendelea kujenga ujuzi na kuwa na mtazamo chanya katika kujifunza na maisha kwa ujumla.
Taaluma
Masomo Yanayofundishwa
Shule ya Sekondari Kajunguti ni shule binafsi inayotoa elimu ya sekondari kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne (I–IV), ngazi ya Ordinary Level (O-Level).
Shule inatoa masomo mbalimbali yanayolenga kumjengea mwanafunzi msingi imara wa kitaaluma, maarifa na ujuzi. Masomo yanayofundishwa ni pamoja na:
1. Kingereza
2. Hesabu
3. Fizikia
4. Kemia
5. Biologia
6. Jografia
7. Kompyuta
8. Historia
9. Historia ya Tanzania na Maadili
10. Kiswahili
11. Business studies
12. Fasihi ya kingereza
13. Kilimo
Mfumo wa ufundishaji
Shule ya Sekondari Kajunguti hutumia lugha ya Kiingereza kama lugha kuu ya kufundishia katika masomo yote, isipokuwa Kiswahili pamoja na Historia ya Tanzania na Maadili, ambayo hufundishwa kwa lugha ya Kiswahili.
Academic Calendar
Kuna mihula miwili ya masomo ambayo ni;
1. Januari hadi Juni
2. Julai hadi Novemba

